Kutengeneza Video Fupi ya AI Ad kwa Duka la Simu za Mkopo – Katoro Mjini

Job ID: 40486922

Budget: $15 – $25 USD

Nahitaji kutengeneza video fupi ya matangazo (sekunde 30) kwa kutumia Canva au programu nyingine ya bure inayotumia AI. Video hii itatangaza duka la simu za mkopo lililopo Katoro mjini, likisisitiza kushuka kwa bei ya kianzio cha kupata simu janja. Nataka video iwe na:
- Picha za mfano za simu za kisasa
- Maandishi ya kuvutia yanayoelezea ofa
- Sauti ya AI ya kusimulia ofa (aina yoyote)
- Animasheni rahisi na mpangilio wa kitaalamu
Nahitaji freelancer mwenye uzoefu wa kutengeneza video za matangazo kwa kutumia picha, sauti, na animasheni za AI, na anayeweza kutoa ushauri wa ubunifu na uhariri wa video.